Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kujenga Nyumba za Makaazi kwa ajili ya Madaktari wa Hospitali za Wilaya

Serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itahakikisha inawawekea makaazi ya karibu watoa huduma wa afya katika Hospitali zote za Wilaya Unguja na Pemba ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi sambamba na kufika kazini kwa wakati

Akizungumza na Mkandarasi pamoja na wasimamizi wa kampuni ya Rans inayojenga nyumba za Madaktar kaitkaH ya Wilaya ya Mwera Pongwe na Kitogani Naibu Waziri Wizara ya Afya Hassan Khamis Hafidh amewataka kusimamia ujenzi huo kua katika hali ya ubora na wenye kiwango

Mkandarasi wa kampuni ya ujens Rans Dkt Mosses Mkonye amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika kwa kipindi cha miez miwili sambamba na kuhakikisha ujenz wa mradi huo uatakua na ubora wa hali ya juu

Akisisitiza upatikanaji wa fedha Mkandarasi kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Amina Habibu amesema ipo haja kwa Wizara ya Fedha kuharakisha upatikanaji wa fedha ili kuhakikisha ujenzi huo unamaliza kwa muda uliopangwa

Loading