WAUGUZI wanafunzi wametakiwa kuwajibika na kuhakikisha kuwa wanaleta mabadiliko makubwa katika fani hiyo ili kuongeza hadhi na sifa za wauguzi hasa kwa walioko makazini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika Mkutano Mkuu wa wa 18 na Kongamano la Kisayansi lilowashirikisha wanafunzi wauguzi katika vyuo vinane Tanzania Bara na Visiwani.
Amesema wauguzi wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika kutoa huduma za afya kwa wananchi, hivyo ni vyema kuongeza nguvu katika kutoa huduma katika mahospitali na vituo vya Afya.
Amefahamisha moja ya kazi za Wauguzi ni kutoa elimu ya afya, kuzuia magonjwa, kutibu, ambapo kwa kufanya hivyo kutasaidia kuondokana na maradhi mengi kwa wananchi na gharama ya matibabu inakuwa ni ndogo.
Amesema katika kuimarisha huduma za Afya hapa nchini Serikali kupitia Wizara ya Afya imejenga Hospitali za Wilaya na Mkoa na sasa nguvu kubwa zimeelekeweza katika kujenga hospitali za Mkoa zilizobali na kuviimarisha vituoa vya afya kuwa vya kisasa ili huduma za afya ziwe zenye ubora wa hali ya juu hapa nchini.
Aidha alisema Wizara ya Afya inafanya kazi kwa ukaribu wa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii lengo ikiwa ni kuwapatia huduma wananchi kwenye ngazi ya jamii na kuibua changamoto zinazowakabili wananchi na kuzifanyia kazi haraka hasa afya ya uzazi na mtoto.
Amewataka wanafunzi hao wanasomea fani ya uuguzi kusoma kwa bidi na kujiendeleza Zaidi ili kuweza kutoa huduma bora za afya hapo baadae.
Kwa upande wake Mkurugenzi Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya Mwanaisha Juma Fakih amesema katikam kuimarisha huduma za Afya hapa nchini wataendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto zote zinazowakabili wauguzi na wakunga kwa lengo la kutoa huduma bora za Afya.
Amesema watashirikiana na Chama cha wanafunzi wauguzi wa vyuo vikuu Tanzania kwa lengo la kutoa wanafunzi waliobora na kuwa na wafanyakazi wzuri hapo baadae.
Akisoma Risalaa mwenyekiti wa jumuiya hiyo Lunemna Athumani amesema Chama chao kinajumuisha vyuo vinane vya Tanzania bara na visiwani vinavyounda chama ambapo ni UNSATA mbayo ilianzishwa kwa dhamira ya kuwakutanisha wahitimu wote wa shahada ya kwanza ya uuguzi na walipo masomoni.
Amefahamisha kuwa malengo cha wanafunzi hao kudumisha umoja ma mshikamano kwa wanafunzi wauguzi wa vyuo vikuu vya Tanzania, kuimarisha utoaji wa huduma kuzingatia ushahidi wa kisayansi pamoja na kuhasisha wauguzi kufanya tafiti ili kuweza kuchangia utoaji wa huduma zenye tija kwa wananchi
Kwa upande wa mwanafunzi Godfrey Denis kutoka Chuo cha afya na sayansi kikuu Shirikishi Muhimbili amesema kutoka na kukua kwa taaluma ya fani ya uuguzi ni vyema wauguzi kufanya tafiti za kutosha ili kuweza kukabilina na maradhi mbali mbali.
Akiwasilisha mada ya afya ya Akili katika mkutano mkuu na kongamano hilo mwanafunzi wa kada ya uuguzi wa chuo cha Zanzibar University Saumu Juma Ali amesema katika kutatua changamoto mbalimbali za afya ikiwemo tatizo la afya ya akili wauguzi wanatakia kutoa huduma za afya kwa ukarimu na upole kuwasaidia wagonjwa.