Waziri Mazrui atembelea kituo cha Blooming Flower of Zanzibar

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuwepo kwa kliniki ya tiba mbadala inayofanya tiba za kutumia njia ya  masaji ya kiafya na viungo itasaidia kwa kiasi kikibwa kuimarisha afya za wananchi wa Zanzibar na wegeni wenye matatizo tofauti ikiwemo waliopata kiharusi.

Waziri Mazrui ameyaeleza hayo huko Mbweni katika kliniki ya Blooming Flower of Zanzibar alipokwenda kufungua na kukagua na kuona jinsi wanavyotoa huduma katika kiliniki hiyo.

Amesema jamii kubwa ya kizanzibari na wegeni wanaofika nchini inakabiliwa na changamoto kubwa ya maradhi ikiwemo waliopata kiharusi, viungo na maradhi mengineyo hivyo kliniki hiyo ya Blooming Flower itaweza kuimarisha afya za wenye maradhi hayo.

Amefahamisha kuwa wahudumu wa kliniki hiyo wanaujuzi mkubwa na vifaa vya kisasa na vya kutosha kwa ajili ya kutoa mhuduma mbali mbali ikiwemo mazoezi, masaji, pamoja kutoa ushauri wa kupunguza uzito na dawa za virutubisho na lishe.

Kwa upande mwakilishi kutoka Kiliniki ya Blooming Flower of Zanzibar amesema wameona ipo haja ya kutoa huduma ya masaji ya kiafya na viungo hapa  hapa Zanzibar kutokana na wananchi wengi wanasumbuliwa na maradhi mbalim mbali.

Amefahamisha kuwa huduma wanazotoa ni za kitaalamu na wanatuamia vifaa maalumu kubaini maradhi na kuweza kuyapatia tiba ambayo inamanufaa makubwa na kuondokana na madhara yaliyotokana na matumizi ya vyakula na dawa mbali mbali.

Loading