Waziri Afya Zanzibar amesema Taasisi za kidini zina nafasi kubwa katika kuisaidia Serikali juu ya utoaji wa huduma za afya

Waziri wa   Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui   amesema kuwa Taasisi za kidini zinanafasi kubwa katika kuisaidia Serikali juu ya utoaji wa huduma za afya  kwa wananchi wake.

Waziri Mazrui ameyaeleza hayo huko Hoteli ya Golden Tulip alipofungua mafunzo ya Uongozi kwa Viongozi wa Hospitali za KKKT yaliwashirikisha viongozi wa vituo vya Afya, wafanyakazi na washauri wa kurugenzi za afya ya KKKT, na vingozi wa vyui vya hospitali za KKKT

Amesema uongozi na usimamizi ni sehemu muhimu ya mfumo wa sekta ya Afya na unasaidia kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali, maamuzi bora na uanzishwaji wa miundo sahihi ya utawala.

Amefahamisha kuwa mafunzo hayo yatasaidia viongozi wa sekta ya Afya katika hospitali na vyuo vya KKKT kuongeza ujuzi na zana muhimu za kukabiliana na changamoto wanazokumabana nazo katika kutoa huduma za Afya na huduma kuwa zenye ubora katika nchi ya Tanzania.

Aidha alisema Zanzibar imepata maendelea makubwa juu ya utoaji wa huduma katika miaka ya hivi karibuni ambapo aliwaelezea viongozi hao kuwa wamefanikisha miundo mbinu ya huduma za afya, kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa muhimu na kuimarisha nguvu kazi ya afya.

Amewataka kuzidi kukuza ushirikiano kati ya wataalamu wa afya wa hospitali za KKKT na Wizara ya afya Zanzibar kuja kuekeza katika sekta ya afya kwa lengo la kuimarisha huduma hapa nchini huku akisisitiza kuangalia makundi maalumu kwenye jamii katika utoaji wa huduma ikwiemo wazee, watu wenye magonjwa sugu, watoto pamoja na mama wazito.

Kwa upande wake Mkurugenzi Huduma za Afya Kanisa Katoliki Tanzania KKKT Dkt Paul Zebadia Mmbando amesema huduma zinazotolewa kwa jamii ambazo zimo ndani ya taasisi yao hazinagalii Dini yoyote na mtu anapofika hupatiwa huduma  ipasavyo na wanatoa na huduma zaidi wanzitoa vijijini.

Amefahamisha kuwa tasisi yao imeweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo na wapo katika mikoa tofauti nchini Tanzania na wanafanya kazi karibu na Serikali na ina jumla ya tasisi za afya 172, tasisi  za kielimu 120 na wanajumla ya  hospitali 24 na vituo vya afya vitavyo 148.

Nae Mratibu wa tafiti na machapisho kutoka TAMISEMI Dkt James Ngekia amesema mafunzo hayo yanayoendelea kutolewa kwa wataalamu hao yamejikita zaidi katika kupata miongozo ya kisera kwa vingozi hao pia kupitia maeneo yanayolingana na matwakwa ya Shirika la Afya ulimwenguni WHO.

Taasisi ya KKKT inafanya kazi na Serikali pamoja na Mashirika ya kitaifa na kimataifa na sasa imetimiza miaka 30 tangu kunzishwa.

Loading