Wataalamu wa Maabara wametakiwa kufanya uchunguzi wa maradhi kwa kufuata utaalamu uliopo duniani

WATAALAMU wa Maabara wametakiwa kufanya uchunguzi wa maradhi kwa kufuata utaalamu uliopo duniani kote ili kuweza kutolewa   tiba sahihi kwa wagonjwa.

Akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo wataalamu wa maabara Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Salim Slim amesema wataalamu hao wanajukumu kubwa la kuchunguza maradhi kwa kina na kuweza kupatikana kwa tiba ya mapema kwa mgonjwa na kuondokana na maradhi.

Amesema katika kufanikisha utaalamu wa Maabara ni vyema wataalamu hao kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ili kuweza kuondokana na mapungufu katika utendaji wa kazi zao za kila siku ambazo zinahitaji utaalamu Zaidi.

Amefahamisha katika kuimarisha utendaji wa kazi za Maabara, Wizara ya Afya inafanya jitihada maalumu za kuziunganisha kimifumo maabara zote hapa nchini ili  ziweze  kukabiliana na maradhi yakiwemo  ya miripuko.

Kwa upande wa Mwakilishi kutoka Jhpiego Joackim Nyarigo  amesema Taasisi yao inafanya karibu na Wizara ya Afya katika kufanikisha kazi mbali mbali ikiwemo masula ya Maabara.

Amesema katika kutekeleza mradi huo wa  huduma za Maabara  awali walitembelea maabara zote zilizomo katika vituo vya afya Unguja na Pemba pamoja na maabara za mifugo ambapo wa walingalia changamoto zilizopo na kuweza kuzifanyia kazi kwa lengo la kuziimarisha maabara hizo.

Loading