WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kupambana na maradhi ya Malaria na kuhakikisha kuwa yanaondoka hapa nchini

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kufanya jitihada kubwa ya kupambana na maradhi ya Malaria na kuhakikisha kuwa yanaondoka hapa nchini.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyaeleza hayo wakati alipofanya mazungumzo na Balozi Maalumu kutoka Taasisi African Leaders Malaria Alliance (ALMA) alipofika ofisini kwake Vuga

Amesema Wizara ya Afya kwa kushirikina na Washirika wa Maendeleo mbali mbali wanafafanya jitihada za makusudi kuona kuwa malaria yanaondoka kabisa hapa nchini ambapo tayari zipo nchi nne kwa Afrika wamefikia kiwango cha kundosha Malaria katika nchi zao.

Amefahamisha kuwa Zanzibar ni nchi ambayo inategemea sana Utalii na nguvu kazi ya wananchi, hivyo ni muhimu sana kuona kuwa maradhi ya Malaria yanaondoka hapa nchini kama nchi nyengine waliofanikiwa kuondosha maradhi hayo.

Amesema Wizara ya Afya kupitia Programu ya kumaliza Malaria wanafanya kazi pamoja na Taasisi ya ALMA na kuja kwa Balozi huo Maalumu kutoka Taasisi ya hiyo ni kutokana ushirikinao uliopo ambapo katika maadhimisho ya mwaka huu wamejipangia kufanya mambo mbali mbali ikiwemo ugawaji wa vyandarua nchi nzima na kufanya mambo mengine

Alisema katika kufikia mpango mpya wa kupambana na Malaria Waziri Mazrui amewata  wananchi wote kushiriki kikamilifu katika juhudi za kutokomeza Malaria hapa nchini ambapo baraza la umoja wa malaria Zanzibar litaundwa ambalo litashirikisha Mashirika mbali mbali Serikali NGOS na wananchi ambao mpango huo umefanikiwa katika kuondosha malaria katika nchi mbali mbali.

Kwa upande wake Balozi Maalumu kutoka Taasisi ya African Leaders Malaria Alliance (ALMA) Anthony Okara++ amesema wataendeleza mashirikiano na Zanzibar katika kupambana na Malaria ili maradhi hayo yanaondoka hapa nchini.

Amefahamisha kuwa Zanzibar inafanya jitihada mbali mbali za kuondosha malaria, hivyo Taasisi hiyo itaunga mkono jitihada hizo ili Malaria isiwe tatizo katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Loading