Katibu Mkuu Wizara ya Afya amewataka Wauguzi na Wakunga kusimamia kazi zao pamoja na kufanya kazi kwa uweledi

UONGOZI wa Idara ya Uuguzi na Ukunga umetakiwa kusimamia na kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara katika Mahospitali na Vituo vya Afya ili wafanyakazi waweze kutoa huduma zenye ubora.

Akizindua Kamati ya ushauri katika Idara ya Uuguzi na Ukunga Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Fatma Mrisho amesema iwapo kutakuwa na usimamizi na ukaguzi kwa Wauguzi na Wakunga katika sehemu zao za kazi kutaondokana na malalamiko kwa wananchi wanaofika kupata huduma za afya.

Amesema Idara ya Uuguzi na Ukunga kwa kushirikiana na Baraza la Uuguzi na Ukunga wanawajibu wa kuimarisha utowaji wa huduma katika Hospitali na vituo vya Afya kwa kutatua changamoto zilizopo ikiwemo, vifaa taaluma na uhaba wa wafanyakazi  na kufanya tafiti mbali mbali na kuweza kuzifanyia kazi.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya Mwanaisha Juma Fakihi amesema fani ya uuguzi na ukunga ni muhimili wa Hospitali na vituo vya afya na kazi kubwa wanazifanya katika kuwahudumia wananchi.

Amefahamisha kutokana na kukua kwa kada hiyo wameona ipo haja ya kuunda kamati ya ushauri ambayo itaweza kushauri mambo mbali yakiwemo masula mazima ya taaluma pamoja na kuratibu mafunzo ya kujiendeleza katika taaluma na kutoa huduma bora kwa jamii.

Amesema Idara ya Uuguzi na Ukunga imeundwa kutokana na umuhimu wake kwa lengo la kutoa huduma bora kwa jamii na kwa sasa inatakiwa kutendewa haki kada ya uuguzi na ukunga na kuweza kubadilisha mfumo mzima wa utoaji huduma Wizara ya Afya.

Kwa upande wa mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga Tanzania Paul Magesa amesema watashirikiana na Zanzibar katika kuhakikisha kazi za Uuguzi na Ukunga zinatekezwa

Amesema Zanzibar Wauguzi na Wakunga wakiweza kusimama vizuri watasadia kufanikisha mambo mengi ya kuleta maendelea na kuondokana na malalamiko kwa wanakwenda kupata huduma za Afya mahospitalini na Vituo vya Afya.

Katika Hatua nyengine Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amefanya mazungumzo na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi na Ukunga Tanzania Bara Paul Magesa na kuahidi kuwa na Mashirikino na Wizara ya afya Zanzibar hasa katika fani ya Uuguzi na Ukunga.

Loading