Chuo kikuu Cha haukland kujenga maabara ya kufundishia Zanzibar

CHUO kikuu cha Haukland  cha nchini Norway kinatarajia kujenga Maabara ya kufundishia hapa nchini ambayo itakuwa na uwezo wa kuwafundisha wanafunzi mbali mbali wa ndani na nnje ya nchi.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Maabara hiyo itajengwa katika maeneo ya Lumumba na ujenzi wake utagharimu shilingi milioni mia nane na utachukua kipindi cha mwaka mmoja hadi kumalizika kwake na utajengwa na kampuni ya Rans.

Amesema kituo hicho maalumu kitakuwa cha aina yake na wakufunzi watakakuwa wa hapa Zanzibar na nnje ya nchi na wanafunzi wa hapa Zanzibar wataweza kufaidi mafunzo kwa walimu walioko nnje ya nchi na watasoma kwa njia ya mtandao.

Amefahamisha katika kufanikisha ujenzi huo chuo kikuu cha nchini Norway na Kampuni ya Rans imetiliana saini mkataba wa ujenzi huo ili kuweza kuanza mara moja kujegwa kwa maaara hiho ambayo itaweza kutoa mafuzo ya muda mrefu na muda mfupi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo kikuu cha Haukeland cha nchini Norway John Dahl amesema wameona ipo haja ya kujenga maaara hiyo kwa Zanzibar ambayo itaweza kufanikisha kuwafundisha wanafunzi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi na kuweza kutoa matokeo mazuri.

Amesema wataedelea kushirikiana na Zanzibar katika sekta ya Afya kwa lengo kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa kutoa taaluma pamoja na huduma za afya.

Katika hatua nyengine Waziri Mazrui amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Marekani ambao umefika na kufanya mazugumzo na kuonesha nia ya kuekeza katika huduma za afya.

Ujumbe huo umesema utaekeza kwa kuja kujenga hospitali ambayo itatoa huduma mbali mbali ikiwemo Magonjwa ya moyo, maradhi ya Mifupa nna mikojo.

 

Loading