Baraza la Uuguzi na Ukunga limefanya ukaguzi Chuo cha Afya Cha Empirial kilichopo kisauni Zanzibar

Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Amina Abdulkadir amesema kuwepo kwa vyuo vyenye kukidhi vigezo vya kusomeshea fani ya uuguzi na ukunga hapa nchini kutasadia kutoa wataalamu wenye ubora wa kuhudumia wananchi.

Amesema faini ya uuguzi na ukunga inahitaji taaluma yeye kiwago cha hali ya juu amayo itamuwezesha mwanafunzi kuwa na uwezo mkubwa wa masomo yake ili baadae aweze kutoa huduma zenye ubora kwa wagonjwa.

Hayo yamefahamika kufuatia ziara maalumu iliyofanywa na Baraza la Wauguzi na Wakunga iliyofanya katika chuo cha afya za sayansi Empirial kilichopo kisauni kuona kiuhalisia wanavotoa taaluma hiyo.

Amefahamisha kuwa Zanzibar hivi sasa kuna vyuo vingi vinavotoa fani ya Uuguzi na Ukunga ambapo baraza linatakiwa kuwafanyia ukaguzi wa mara kwa mara wa kuona namna gani wanatoa taaluma kulingana na matakwa ya Serikali ya kutoa taaluma iliyo na ubora.

Kwa upande wake Mrajis wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Vuai Kombo Haji amesema kati ya kazi za uguuzi na Ukunga waliyonayo Baraza  ni kuangalia mafunzo yanayotolewa na vyuo vinavyosemesha Uuguzi na Ukunga , idadi ya walimu wanasomesha mafunzo hayo, pamoja na kuangalia mtaala wa kufundushia pamoja na kuona ithibati juu ya mafunzo hayo.

Alifahamisha kwa upande wa chuo hicho cha Afya cha  Empirial Baraza limeridhishwa na taaluma inayotolewa na chuo hicho na kuwataka kuendelea kutoa kuzidi kufanikisha taaluma hiyo ili kutoa wanafunzi wenye ubora wa hali ya juu.

Nae Mjumbe wa Baraza la Uuguzi na Ukunga kutoka Afisi ya Mwanasheria Mkuu Salim Mohamed Abdalla amesema kila fani inaumuhimu wake kwa jamii hivyo amewataka wanafunzi wa chuo cha taaluma za sayansi cha Empirial Kutilia maanani juu ya fani waliyoichagua kwa lengo la kuja kutoa huduma zenye ubora.

Amesema maadili ya Uuguzi na Ukunga yanatokana na kuwa na imani katika kuwahudumia wananchi hivyo ni vyema kuwa na maadili mema ya kuwahudumia wananchi pamoja na kutunza siri za wagonjwa na kuhakikisha unatoa msaada kwa mgonjwa bila ya kujali maslahi makubwa ya kazi hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha taaluma za afya cha Empirial Jokha Khamis Juma amesema wamefarijika kutembelewa na ujumbe wa Baraza la Uuguzi na Ukunga ambao unasaidia katika kuimarisha utendaji wa chuo hicho.

Amefahamisha kuwa kwa uapande wa chuo chao wanafanya kila jitihada ya kutoa taaluma zenye ubora ili wanafunzi wawe na kiwango cha kutoa huduma za afya hapo baadae.

Loading