WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuja kwa mradi wa Mmama utasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hapa nchini.
Akizungumza na waandhishi wa wa habari kuelekea uzinduzi wa kupatiwa vifaa vya mama wajawazito kupitia mradi wa Mmama vilivyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation ambavyo vitatolewa huko Kizimkazi na Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Mmama inafanya kazi kubwa na tayari umeshawahudumia akinama elfu moja mia tisa na nne katika vituo vya afya Unguja na Pemba.
Amefahamisha kuwna mradi wa Mmama umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vitonavyo na uzazi na kuweza akina mama kufika kwa wakati vituo vya Afya wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Zuwena Fara amesema kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, USAID na Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wameshirikiana kuunda mfumo maalumu wa kuwasaidia akina mama wenye matatizo ya uzazi na hutumia njia simu ili kurahisisha kupata huduma kwa wakati.
Amesema tangu kuanza kutumia mfumo huo ambao umezinduliwa rasmi mwaka jana Dodoma na walieka pailot Shinyanga na wameweza kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 40 na kwa Zanzibar umeanza kutumika mwaka huu na ifikapo mwezi wa tisa utatumika Tanzania nzima.
Nae Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswad amesema mfumo wa Mmama kupitia kampuni yao ya Vodacom inafanya kazi kwa ukaribu na mfumo unamilikiwa na Serikali na lengo kubwa kuwezesha akina mama wajawazito wafike kituo cha Afya kwa usalama na waweze kujifungua kwa usalama.