Hii inahusisha utoaji wa huduma za kinga na elimu ya afya zikiwemo huduma za afya ya mama na mtoto, huduma za kudhibiti VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma, huduma za Kumaliza Malaria Zanzibar, pamoja na huduma za Lishe.
Utoaji wa elimu kuhusu maradhi ya mripuko kama vile Kipindupindu na ibola, kwenye maeneo husika na kutoa tahadhari kwa jamii kwa ujumla namna ya kujikinga na maradhi hayo.
Utoaji elimu ya Afya, Afya ya Mazingira, huduma za ufuatiliaji mienendo ya maradhi, Afya ya wafanyakazi, huduma za maradhi yasiyoambukiza, huduma za maradhi yasiyopewa kipaumbele (Negleted Tropical Diseases- NTD), huduma za afya ya akili ya msingi, huduma za afya ya macho ya msingi na huduma za afya Bandarini na Uwanja wa Ndege.