Maana:
Ni kinga inayo tolewa kwa viumbe hai kujikinga na maradhi ya kuambukiza. Chanjo kawaida hutolewa kwa kiumbe hai kabla ya kupata maambukizo. Haitolewi kwa alie tayari ameambukizwa, badala yake anahitaji apate matibabu mengine na si chanjo tena.
Wizara ya Afya Zanzibar inatoa chanjo aina tatu (3). Nazo ni:-
- Chanjo ya Homa ya manjano
- Chanjo ya homa ya Ini
- Chanjo ya homa ya uti wa mgongo
Chanjo ya Homa ya manjano
Chanjo hii hutolewa Wizara ya Afya Zanzibar kwa Zanzibar na sio pengine popote. Chanjo hii ni maalumu kwa wasafiri ambao wanasafiri kwenda nje ya nchi. Msafiri ambae anaehitaji chanjo hii anatakiwa apatiwe chanjo hii siku kumi (10) kabla safari.
Chanjo hii inatolewa siku tatu (3) katika wiki, mda wake ni saa moja na nusu asubuhi.
Ili kupata chanjo hii muhusika anatakiwa aje na kivuli au hati halisi ya kusafiria. Chanjo hii kwa alie patiwa inakua kinga ya maisha yote (kwa alie chanjwa 2018).
Chanjo ya homa ya Ini
Hii hutolewa siku zote na kwa mtu yeyote. Muda ni saa moja asubuhi hadi saa nne asubuhi. Huduma hii hupewa kwa kuja na majibu ya hospital ambaya yanaonesha hujapata maambukizi ya homa ya ini. Kama tayari ushapata maambukizi hutapata chanjo hii, badala yake utatakiwa uendelee na matibabu hospitalini. Chanjo hii ina awamu tatu (3):-
- Awamu ya kwanza ni kwa mwenzi mmoja wa mwanzo
- Awamu ya pili ni kwa mwenzi wa pili unaofuata
- Na awamu ya tatu inafanyika baada ya miezi mitatu (3) au sita kupita
Muhusika akisha pata chanjo dozi zote tatu (3) atakua na kinga kwa muda wa miaka 20.
Homa ya uti wa mgongo
Hii tunaweka kinga kwa mtu mmoja mmoja au kwa makundi, inatolewa kila siku, saa moja hadi saa nne. Hii hahihitaji majibu kutoka hospitalin wala kuwa na hati yeyote. Kinga yake ni muda wa miaka mitatu.
WASAFIRI WOTE WANAOKWENDA NJE YA NCHI WANATAKIWA KUCHANJA CHANJO ZA SAFARI
Siku za huduma ya chanjo ni Jumatatu – Jumatano – Ijumaa
Unatakiwa kuchanja siku 10 kabla ya safari.