Ziara ya Waziri wa Afya Zanzibar – Tumbatu

SERIKALI ya Mapindi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya,  imesema inafanya kila aina ya jitihada kuona kuwa Tumbatu inapata maendeleo mbali mbali yakiwemo ya  sekta ya afya.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui  huko Tumbatu wakati alipofanya ziara ya kuangalia eneo la ujenzi wa Hospitali ambao utachukua kipindi cha mwaka mmoja hadi kumalizika kwake kwa mujibu wa makataba.

Amesema Mkandarasi aneshughulikia ujenzi Hospitali ya Tumbatu anamalizia hatua za mwisho ujenzi wa Skuli na mara baada kukamilisha ataanza ujenzi wa Hospitali ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa wakazi wa kijiji hicho.

Amefahamisha kuwa katika kufanikisha ujenzi wa Hospitali hiyo mkandarasi anatakiwa kuvunja mara moja jengo la zamani na kuwezesha kufanikisha ujenzi huo kwa ufanasi na kusema kuwa atafanya ziara kila baada ya miezi mitatu kungalia maendeleo.

Kwa upande wa Mkandarasi wa ujenzi huo John Simon wa Kmpuni ya Simba Developer Limited  Amesema wapo katika maandalizi ya kuanza ujenzi wa Hospitali hiyo na watahakikisha ujenzi huo unamaliza kwa wakati uliopangwa.

Kwa upande wa wakaazi  wa kijiji hicho wamesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali katika kijiji  hicho  utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kupata huduma za Afya kwa uhakika  hasa mama wajawazito.

Amesema kwa sasa mama wajawazito na wenye matatizo mengine  anapopta shida inabidi wakodi boti na wavuke  jambo ambalo husabaisha muda kuwa mkubwa bila ya kupata huduma na kumtaka waziri wa Afya mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo waajikriwe wafanyakazi wazawa wa kijiji hicho.

Katika hatua nyengine wananchi wa Kijiji cha Nunwgi wamefurahiswa na hatua ya Serikali kupitia Wizara ya Afya kukijenga upya kituo cha Afya katika kijiji hicho baada ya kuwa kimechakaaa

Walisema hatua hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa kupata huduma za afya kwa ukaribu na kuepukana na usumbufu wanaoupata kwa sasa kuzifata huduma hizo mbali.

Kituo cha Afya Nungwi kimekuwa hakifanyi kazi kwa kipindi cha miaka mitatu sasa baada kuwa kichakavu  na wananchi wanakwenda kupata huduma katika kituo cha Afya Maafa.

Loading