Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikiana na Brazil kuimarisha Sekta ya Afya Nchini

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itashirikina na Brazil kuimarisha sekta hasa katika huduma za afya ya mama wajawazito na watoto.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika mkutano na ujumbe kutoka Wizara ya Afya ya Brazil na Taasisi ya Brazilian Funding Cooperation Agency (ABC) uliwashirikisha uongozi wa Wizara hiyo pamoja na Balozi wa mdogo wa Brazil aliyepo hapa nchini.

Waziri Mazrui amesema katika kukabiliana na vifo vitokanavyo na uzazi Wizara ya Afya imejipanga kwa kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kuimarisha huduma vituo vya afya na Hospitali za Wilaya na Mkoa pamoja na kufanya kazi kwa kushirikina na wahudumu wa afya wa kujitolea ngazi ya jamii.

Amefahamisha kuwa hatua ya kuja kwa ujumbe huo utasaidia kuwasomesha wafanyakazi, kubadilishana uzoefu nchini Brazil na Zanzibar kwa lengo la kukabilina na vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Ujumbe huo upo hapa Zanzibar kwa muda wa wiki moja kuangalia namna gani ya kushirikiana katika masuala ya kuimarisha huduma za afya kwa mama wajawazito na watoto wachanga na watapata furasa ya kutembelea vituo vya Afya vya Unguja na Pemba.

Katika hatua nyengine Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Big win kutoka nchini Uengereza ambao unafanya kazi kubwa ya kukuza watoto wenye vipaji.

Amesema watoto wanahijati kupatiwa malezi bora ili waweze kuwa na akili nzuri na vipaji ambayo vitasaidia katika kuimarisha afya zao sambamba na kuwa na watoto watakaosaidia mambo mbali mbali hapo baadae.

Kwa upande wa Muakilishi kutoka Tasisi ya Big win ya nchini Ungereza amesema taasisi yao inafanya kazi katika nchi tofauti kwa lengo la kuinua vipaji vya watoto katika nchi husika.

Amesema kwa hapa Zanzibar watahakikisha wanashirikiana na Sekta ya afya, Wizara ya Elimu na Wizara ya Maendeleo ya Jamii wazee Jinsia na watoto kwa lengo la kuinua vipaji hapa nchini.

Loading