WIZARA ya Afya Zanzibar imekusudia kuimarisha mifumo yake ya uagizaji dawa vifaa tiba, usambazaji na uhifadhi wa dawa katika Bohari zake za  Unguja na Pemba

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema kuwa imekusudia kuimarisha mifumo yake ya uagizaji dawa vifaa tiba, usambazaji na uhifadhi wa dawa katika Bohari zake za  Unguja na Pemba kupitia wataalamu kutoka nchini Afrika ya Kusini kupitia Shirika la misaada la Marekani USAID.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui alipokutana na kufanya mazungumzo na wataalamu kutoka Afrikayakusini kupitia shirika la misaada la Marekani USAID ambao wapo nchini kwa lengo la kusaidia kuimarisha mifumo ya uagizaji dawa, vifaa tiba usambazaji na uhifadhi wa dawa .

Amesema hatua hiyo ya kuimarisha mifumo inakuja baada ya Wizara ya Afya kuifanyia kunzisha Sheria ya Wakala wa Bohari kuu ya Dawa ambayo tayari imesomwa kwa mara ya kwanza Baraza la Wawakilishi ambapo matarajio ya sharia hiyo itakuwa tayari mwaka 2024.

Amefahamisha kuwa baada ya kukamilika kwa sharia hiyo itawapa mamlaka kamili Bohari kuu ya Dawa zote na vifaa tiba vyo kwa Zanzibar itakuwa na Maghala Unguja na Pemba pamoja na kuwa na majukumu ya kuagiza dawa na vifaa tiba vyote na pamoja na uhifadhi na kusambaza kwa utaratibu wa mifumo iliyokuwa na ubora wa hali ya juu.

Aidha alisema kuwa, ili kuweza kuwa na Bohari yenye sifa bora ni lazima iwe na mifumo yakimataifa inayotambulikana hivyo Wizara ya Afya itahakikisha inaimarisha mifumo yake kwa lengo la kutoa huduma nzuri za dawa pamoja na vifaa tiba na kulitaka Shirika la kimarekani USAID kusaidia kutengeneza mambo yote muhimu yanayohusiana na Bohari kuu ya Dawa kuwa wakala.

Katika hatua Nyengiene Waziri Mazrui amefanya Mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia na kuzungumzia masuala mazima ya sekta ya afya ikiwemo kuimarisha huduma za Afya ya msingi pamoja na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ambao utawasili mwanzoni mwa mwezi wa Novemba kuja kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa.

Loading