Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amewapa Pongezi Taasisi ya The Same Qualities Foundation ya Arusha kwa kusaidia kuimarisha Afya za wananchi Nchini

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesifu jitihada za Taasisi ya The Same Qualities Foundation ya Arusha kwa kusaidia katika kuimarisha Afya za wananchi Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa kuwafanyia upasuaji wa midomo wazi.

Amesema kwa Zanzibar tayari wamefika katika awamu tofauti na kuwafanyia upasuaji wa midomo wazi watoto na watu wazima na kufanikiwa kuwarejeshea tabasamu ambapo kwa awamu hii ya sita jumla ya watu 13 wamefanyiwa upasuaji huo.

Amefahamisha kuwa kutokana na jitihada wanazofanya  taasisi hiyo Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana katika kuimarisha afya za wenye matatizo ya midomo wazi kwa kuwapatia matibabu kupitia wataalamu kutoka nchi mbali mbali.

Aidha amesema upasuaji huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa awali wenye midomo iliyopasuka walikuwa wanashindwa kunyonya na kula vizuri ambapo mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo watot hao wanaendelea vizuri na wanaweza kunyonya na kutoa wito kwa wenye matatizo hayo ambao midomo yao imepasuka nnje au ndani kufika hospitalini kwa kupatiwa matibabu.

Kwa uapande wake Dkt Samuel Siseja kutoka The Same Qualities Foundation amesema waliona wagonjwa wenye matatizo ya midomo wazi wapatao kumi na tano na wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji watu 13 na hali zao zinaendelea vizuri na wawili wahawakufanikiwa kutokana na changamoto mbali mbali za kiafya watawafanyia awamu nyengine.

Amesema miongoni mwa waliofanyia upasuaji alikuwemo mama mwenye umri wa miaka 37 na mtoto wake wa miezi sita ambao wote kwa pamoja walikuwa na changamoto ya midomo iliyopasuka kwa ndani na mwengine 27 na hali zao wote zinaendelea vizuri.

Ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwakaribisha na kuwapata ushirikiano wa kurejesha tabasamu kwa watoto na watu wazima wenye matatizo ya midomo wazi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.

Loading