Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la USAID ili kuweza kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.
Amesema Shirika la USAID limekuwa likisaidia Sekta ya Afya katika Nyanja tofauti ikiwemo Malaria, Kifuakikuu, homa ya Ini na huduma nyengine za kijamii.
Akizungumza na Mshauri Mkuu wa Shirika la USAID Magret Toylor huko ofisini kwake Mnazimmoja Waziri Mazrui amesema kutokana na jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Washirika wa Maendeleo mbali mbali wakiwemo USAID Wizara ya Afya imeweza kupiga hatua katika kupambana na Malaria ambapo kwa sasa yapo chini ya asilimia moja.
Amefahamisha kuwa USAID imeweza kusaidia katika kudhibiti ugonjwa wa ukimwi ambayo yameathiri sana ambayo yanaathiri sana nguvu kazi ya watanzania ambapo kwa sasa UKIMWI hapa Zanzibar umepungua kwa kiasi kikubwa wamefikia malengo ya 90, 90, 90 na Wizara inafanya jitihada ya kufikia malengo ya 95, 95 na watoto wachanga wanaozaliwa na UKIMWI wamepungua sana.
Aidha alifahamisha kuwa bado homa ya ini pamoja na maradhi ya Kifua kikuu yanasumbua sana wazanzibari na yanagharama kubwa kuyatibu, hivyo amewataka washirika maendelea mbali mbali ikiwemo USAID kuendeleza misaada yao kwa wananchi wa Zanzibar pamoja na vifaa tiba na mafunzo kwa wafanyakazi wake.
Kwa upande wake Mshauri Mkuu wa Shirika la Misaada la USAID Magret Toylor amesema Shirika lake litaendeleza Misaada yake kwa Zanzibar ili kuweza kuimarisha huduma za afya.
Amesema lengo lengo la kufanya ziara hapa nchini nikutembelea vituo vya Afya na jumuiya wanazozisaidia .
Katika hatua nyengine Waziri Mazrui amekutana na watendaji wa Willow International na kuahidi kufanya kazi kwa pamoja na Wizara ya Afya ili kuweza kuimarisha huduma za kijamii.