Usajili na leseni za Afya

Huduma hii ya usajili kwa wauguzi, wakunga, Madaktari, Watoaji huduma za Afya pamoja na watoaji wa tiba mbadala na tiba asili wote kwa pamoja husajiliwa na kupatiwa liseni na wizara ya Afya kwa utaratibu ufuatao.

Huduma za Uratibu wa Wauguzi na Wakunga. Baraza la wauguzi na wakunga ndilo linalohusika na usajili na utoaji wa liseni kwa wauguzi na wakunga wote wanaofanya kazi katika vituo vyote vya Afya Zanzibar na nje ya Zanzibar ambao wamesajiliwa na baraza hili. Baraza hili pia wanahusika na ufuatiliaji wa utendaji kazi kwa wauguzi na wakunga wote wafanyao kazi katika vituo vya Afya ambao wamesajiliwa na baraza hili.

Huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala. Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala ndio baraza lenye mamlaka ya usajili na utoaji liseni kwa watoaji Tiba asili na Tiba Mbadala (waganga). Usajili wa kliniki na maduka yatoayo huduma za Afya pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya utumiaji wa dawa zenye viwango na kuwataka waganga wa tiba asili kufata masharti yaliyowekwa.

Huduma za Baraza la Madaktari. Baraza la Madaktari ndilo baraza lenye mamlaka ya usajili na utoaji liseni kwa Madaktari bingwa pamoja Madaktari wasaidizi.

Tahadhari: Ni makosa kisheria kutoa huduma yeyote ya Afya bila kuwa na usajili na liseni kutoka katika baraza husika. Mtu yeyote atakaebainika anafanya hivi hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake.

Loading