Kitengo cha Afya ya Mazingira cha Wizara ya Afya pamoja na wafanyabishara ya vyakula bustani ya Forodhani wamefanya usafi katika sehemu yao ya kufanyia biashara ili kuweza kuwa na mazingira mazuri.
Afisa afya kitengo cha afya ya mazingira Amina Makame amesema katika sehemu ya uuzaji wa vyakula katika enoe la bustani ya Forodhani linakiwa
kuwa usafi wa hali ya juu ikiwemo uhifadhi wa chakula pamoja na uhifadhi wa taka.
Amewataka wafanyabiashara ya chakula katika eneo hilo la foradhani kuuza vyakula vyenye ubora ili kuweza kulinda haiba ya eneo hilo lenye historia kubwa ya Zanzibar.
Kwa upande wa wafanyabiashara hao wamesema wamekuwa na kawaida ya kufanya usafi wa pamoja kwa kila mwezi ili kuweza kuitunza sehemu hiyo.
Wamesema watahakikisha wanatoa huduma zilizobora kwa kuuza vyakula vyenye kiwango ili kukuza sifa ya eneo la Forodhani.