Taasisi ya NED kusaidia kufanya matibabu ya Magonjwa ya Kichwa, Uti wa Mgongo na Mishipa ya hisia katika Hospitali ya Mnazimmoja

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema   Taasisi ya NED imeweza kusaidia kufanya matibabu ya magonjwa ya kichwa, uti wa mgongo  na mishipa ya hisia katika hospitali kuu ya mnazimmoja na hadi kufikia sasa zaidi ya kambi 200 zimefanyika na kufanikiwa kuwafanyia upasuaji zaidi wagonjwa elfu tatu.

Akifungua mafunzo ya uchunguzi wa ubongo wa mwandamu yaliwashirikisha madaktari kutoka nchi mbali mbali na wahapa nchini Waziri Mazrui amesema madaktari kutoka nchini Spain pamoja na madaktari wa nchi nyengine kwa kushirikiana na wahapa nchini wameweza kuwafanyia upasuaji wananchi wa Zanzibar wenye matatizo mbali mbali

Amesema matatizo hayo ni pamoja na upasuaji mkubwa wa vichwa, mgongo, na magonjwa ya kuzaliwa nayo kwa kushirikiana na Tasisi ya NED ambayo inaendelea kugharamia vifaa tiba zikiwemo microscope ya kufanyia upasuaji na dawa ambapo karibu dola milioni mbili zimetumika.

Aidha alifahamisha kuwa tasisi ya NED kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazimmoja imeweza kupata kibali na kuruhusiwa kuanzisha masomo ya Neurosurgery na kwa sasa tayari wanao wanafunzi wenyeji na wageni kutoka nchi mbali mbali wanaofanya mzunguko wao wa kimasomo katika hospitali ya Mnazimmoja.

Waziri Mazrui amesema idadi ya madaktari bingwa wa upasuaji  wa Kichwa, uti wa mgongo na mishipa ya hisia imeongezeka kutoka Daktari mmoja mwaka 2015 na kufikia mabingwa wane mwaka 2023 na wengine watatu wakitarajiwa masomo yao hivi karibuni

Kwa upande wake Mkuu wa Skuli za Afya na Sayansi za Tiba SUZA Dkt Salma Abdi Mahmoud amesema wameshukuru kupata fursa ya   kushirikiana na taasisi ya NED Foundation na Wizara ya Afya katika kuendeleza tathnia ya afya.

Amesema katika mafunzo hayo wanazadi ya wanafunzi wa 32 ambao wameungana na madaktari kutoka Mnazimmoja na kujifunza kivitendo na taaluma inayotolewa na madaktari kutoka nchini Spain.

Taasisi ya NED imeanza kufanya kazi tangu Novemba mwaka 2014 na kufunguliwa  mwaka 2015 na rais wa awamu ya saba na hadi sasa taasisi imetimiza maika tisa na kuweza kupata mafanikio kadhaa na tasisi hiyo inafanya kazi zake kwa mashirikiano makubwa na madaktari wazawa na wakigeni ambapo Zaidi ya madaktari 851 wa kigeni kutoka mbali mbali duniani kama vile Spain, Marekani, Germany, Chile na kenya wameshakuja kufanya kazi na taasisi hiyo.

Loading