Waziri Mazrui amefanya mazungumzo na hospital ya Benjamin Mkapa

Waziri wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara ya Afya ipo tayari kushirikiana na Hospital ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma katika kutoa huduma mbali mbali za matibabu.

Amesema kutokana na huduma za matibabu wanazozitoa hospital hiyo ni zenye ubora zaidi Wizara ya Afya itafanya mashirikiano ili kuweza kupeleka wagonjwa walioshindikana kupata matibabu.

Waziri Mazrui ameyasema hayo huko ofisini kwake alupofanya mazungumzo na ujumbe kutoka hospital ya Benjamin Mkapa iliyopo Dododma walipofika kujitambulisha.

Amefahamisha kuwa katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na ujenzi wa hospital za Wilaya na Mkoa ili kuweza kuimarisha huduma za afya hapa nchini

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Hospital ya Benjamin Mkapa Dkt Anthony Biyunda amesema kutokana na huduma mbali mbali za wanazozitoa hosptalini hapo wameona ipo haja ya kuja Zanzibar kuweza kushirikiana na Wizara Ya afya kwa lengo la kiwahudumia wananchi.

Amesema hospital ya Benjamin Mkapa inatoa huduma za kibingwa kwa kufanya uchunguzi na kutoa Tiba kwa magonjwa yote huku ikijikita zaidi kwa magonjwa yasioambukiza yakiwemo Figo, Moyo, Macho na saratani

Amefahamisha kuwa hospital hiyo inafanya huduma za upandikizaji wa Figo ambapo huduma hiyo ilianza rasmi mwaka 2018 na mpaka Sasa jumla ya watu 27 wameshapandikizwa Figo na wanaendelea vizuri

Loading