WAZIRI WA AFYA MH.AHMED MAZRUI AMUAGA ALIYEKUA MFAMASIA MKUU WA SERIKALI

Waziri wa afya zanzibar nassor ahmed mazrui amesema kuwa mashirikiano mazuri katika kazi yanawezesha kutoa huduma zenye ufanisi kwa umma.

Amesema katika utekelezaji wa huduma mbali mbali za afya  ikiwemo upatikanaji wa  dawa Wafanyakazi sekta ya Afya  wanatakiwa kuwa ushirikiano wa hali juu ili huduma hiyo iwe na ufanisi kwa jamii.

Waziri Mazrui ameyaeleza hayo  katika hafla maalum ya kumuaga aliyekuwa mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na Wafanyakazi wengine wa ofisi hiyo huko katika ukumbi wa ofisi za ZURA.

Amefahamisha kuwa Wizara ya Afya kupitia ofisi ya Mfamasia Mkuu wa serikali inafanya Kila jitihada kuona upatikanaji wa dawa na vifaa tiba zinapatikana katika mahospitali na vituo vya afya ili wananchi waoate huduma.

Aidha, amewataka Wafanyakazi kufanya kazi kwa mashirikiano  na kupendana pamoja  kujenga utamaduni wa kuagana wakati wa mfanyakazi anapofikia kustaafu .

Kwa upande wake MKurugenzi Mkuu wa Wizara Ya afya Dkt Amour Suleiman Mohamed amesema licha ya Changamoto za upatikanaji wa dawa na vifaa tiba Serikali kupitia Wizara ya Afya itafanya Kila jitihada dawa isiwe tatizo katika mahospitali na vituo vya afya.

Mfamasia Mkuu mstaafu Habib Ali sharifu akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Afya Zanzibar Ahmed Mazrui

Nae mfamasia Mkuu mstaafu Habib Ali sharifu amesema mashirikiano katika kazi ndio msingi mkubwa wa kuleta mafanikio hivyo amewataka Wafanyakazi wote Kuna mashirikiano katika sehemu za kazi ili wananchi waoate huduma zenye ubora

Kwa upande wake  mfamasia Mkuu wa serikali Hidaya Juma Hamad amesema kuwa atayaendeleza Yale mazuri yote aliyoacha mfamasia mstaafu na kuendeleza mashirikiano katika ofisi yao  ili huduma za afya ziweze kuwa na ufanisi wa hali ya juu.

 

Loading