Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza ushirikiano wake na China

Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza ushirikiano wake na China kwa lengo la kuimarisha huduma za Afya kwa wananchi pamoja na kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Afya duniani.

Akizungumza kwa Niaba yake, Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika maadhimisho ya miaka sitini ya mashirikiano baina jimbo la jimbo JIANGSU la nchini China na Wizara ya Afya Zanzibar yaliyofanyika huko Golden Tulip amesema China inaendelea kuunga mkono jititada za Serikali za kufanikisha huduma mbali mbali ikiwemo Sekta ya Afya.

Amesema madaktari kutoka China jimbo la Jingsu wamekuwa wakifanya kazi katika hospitali mbalimbali wamesaidia kutoa huduma za baadhi ya maradhi yanayowasumbua nchi ya Zanzibar muda mrefu ikiwemo kichocho malaria pamoja na saratani ya shingo ya kizazi.

Amesema kwenye historia hiyo muhimu ya ushirikiano imeleta mafanikio makubwa ikiwemo kutibu wagonjwa zaidi ya Milioni Nane , kufanya upasuaji wa maradhi mbalimbali kwa wagonjwa Zaidi ya laki mbili pamoja na kuokoa ya wagonjwa wenye maradhi mbali mbali .

Ameongeza kuwa mbali na matibabu madakatari hao wameweza kutoa ujuzi na teknolojia inayotumiwa na madaktari wa Zanzibar zinazosaidia kutibu na kuchunguza maradhi yanayoambukiza na yasiyoyakuambukiza jambo linaloongeza uimara wa sekta ya afya Nchini.

Akizungumzia juu ya maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi amesema mpaka kufikia mwezi Machi mwaka huu Zaidi ya wanawake Ishirini na Sita Elfu wamefanyiwa uchunguzi na waliogunduliwa na tatizo hilo ni Zaidi ya Elfu na Mia Tano ambao waliweza kupatiwa matibabu stahiki na kwa wakati.

Mbali na hayo ameishukuru timu ya madaktari wa kichocho ambao mpaka kufikia mwezi wa Agosti wameweza kufanya uchunguzi wagonjwa Zaidi ya Elfu Sitini katika Shehia Mia Moja na Tisa kisiwani Pemba jambo lililofanikisha kufikiwa asilimia Ziro nukta Sita ya maradhi hayo.

Mhe Hemed amesisitiza kuwa ni wakati wa kufikia malengo ya pamoja kwa kuhakikisha huduma bora za Afya zinafikiwa kupatiwa mafunzo wataalamu wa afya wa kada zote,kuanzisha tafiti za kisayansi na ubunifu kuanzisha miradi ya pamoja ya kutibu magonjwa sugu, matumizi ya teknolojia ya kisasa, kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto, elimu ya jamii ya huduma za kinga sambamba na huduma za afya endelevu.

Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini misaada inayotolewa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ikiwemo dawa, madaktari, vifaa tiba, nyumba za wafanyakazi ambavyo vimekuwa na nafasi kubwa katika kumaliza matatizo yaliyokuwa yakiikumba sekta ya Afya nchini.

Mbali na hayo Mhe. Hemed ameiomba China kuangalia fursa nyengine zilizopo ikiwemo utalii, uchumi wa buluu, mafuta na gesi jambo liatakaloongeza wawekezaji wengi kutoka nchini humo na kuiwezesha Zanzibar kufikia malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Mkuu wa Jimbo la JIANGSU XU KUNLIN ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika maeneo tofauti ya sekta ya afya ili kuona Zanzibar inaweza kufanya matibabu ya kibingwa bila ya kutumia gharama kubwa ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

Amefahamisha kuwa kwa muda waliokuwa wakifanya matibabu nchini wameweza kuleta mageuzi kwenye sekta ya afya jambo linalowahamasiha kuendelea kuleta timu nyengine za madaktari sambmba na kuongeza misaada mbalimbali ya dawa pamoja na vifaa ili kumaliza tatizo hilo katika hospitali zilizopo nchini.

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk Salim Slim ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya ambayo imekuwa na sera bora zinazowawezesha washirika wa maendeleo wakiwemo China, Marekani na nchi nyengine kuleta wataalamu wa afya, vifaa tiba sambamba na kuwapatia mafunzo madaktari wazawa jambo linaloongeza ufanisi wa utoaji wa huduma bora za afya nchini.

Katika maadhimisho hayo Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana saini ya mashirikiano na Hospitali ya JIANGSU sambamba na kupatiwa msaada wa dawa za maradhi mbalimbali.

Loading