Makabidhiano ya Gari kwa Wizara ya Afya Zanzibar

WIZARA ya Afya Zanzibar imejipanga kuimarisha huduma za Afya ya Msingi kwa kuviwezesha vituo vya afya kutoa huduma mbali mbali  kwa wananchi wa Unguja na Pemba.

Akizungumza baada ya kukabidhi Gari na pikipiki kwa Watendaji wakuu wa afya wa Wilaya wa Unguja na Pemba Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema   lengo la kukabidhi Gari hizo ni kuimarisha zoezi la usambazaji wa Chanjo katika vituo vyote hapa nchini.

Amesema watendaji wa maeneo hayo kwa muda wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mengi ikiwemo uhaba wa vifaa fedha usafiri pamoja na taaluma zitakazoongeza ufanisi wa kiutendaji kwa wahudumu wa maeneo Hayo.

Aidha amewaagiza watendaji hao kuvitumia vifaa hivyo walivyokabidhiwa kwa matumizi yaliyokusudiwa ikiwemo kwa kupakiwa  dawa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu nakutoa Imani kwa wafasdhili kuendelea kusaidia kwa vifaa hivyo na vyengina kwa maendeleo endelevu ya sekta hiyo.

Nae Afisa wa Mpango wa Chanjo Unguja Ruzuna Abdulrahim Mohamed amesema kutolewa kwa vifaa hivyo vinakwenda kuongeza ari ya utendaji kwa kubadilisha mwelekeo wa watendaji hao katika zoezi la utowaji wa chanjo pamoja na kuwasaidia watendaji wa afya kuyafikia maeneo yenye uhitaji kwa haraka.

Daktari Dhamana wa Wilaya wa Chakechake Sharif Hamad Khatib amesema lengo la gari hizo ni kumaliza matatizo yanayovikabili vituo hivyo ikiwemo kuboresha afya ya msingi wa huduma za mama na mtoto, usambazajin wa chanjio, ukaguzi wa vituo na watendaji kutoa wa elimu ya afaya kwa jamii pamoja na mambo mengine yatakayoongeza nguvu ya utendaji katika maeneo hayo.

Jumla ya gari 7 na pikipiki 21 zimekabidhiwa kwa vituo vya afya mbalimbali vya Unguja na Pemba ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Afya Zanzibar kupitia ziara aliyoifanya mwezi April 2023 baada ya kutembelea vituo hivyo.

Loading