Kongamano la kumi na moja la Sekta ya Afya linatarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar

Kongamano la kumi na moja (11) la Sekta ya Afya linatarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar na litawashirkisha wataalamu mbali mbali wa ndani na nje ya nchi wa masula ya sekta Afya.

Akizungumza mara baaada ya mkutano wa matayarisho wa Kongamano hilo ambao umewashiriksha kamati ya Tanzania bara na visiwani Rais wa Kongamano hilo Tanzania Health Summit Dkt Omar Chilo amesema mkutano huo utafanyika octoba mosi hadi tatu ya mwaka huu katika viwanja vya ZIFF Fumba.

Dkt Chilo amesema madhumuni ya Kongamano hilo ni kuwakutanisha wadau sekta ya Afya wapatao zaidi elfu moja na mia tano na nchi 12 zitashiriki ambao wamegawanyka katika Nyanja tofauti za Afya wenye lengo la kuimrisha mifumo ya afya Tanzania.

Aidha amefahamisha kuwa Katika kongamano hilo mada mbali mbali zitajadiliwa zikiwemo masuala mazima ya Rasilimali watu, huduma za afya kwa sekta binafsi na huduma bora za Afya na mada nyengine.

Aidha alisema matokeo ya kongamo la Afya ni makubwa kutokana na kuwa linakutanisha wadau wengi zaidi wa sekta ya afya na kutatua changamoto mbali mbali zinazo ikabili sekta ya afya.

Kwa upande wa mjumbe wa kamati ya maandalizi ambae anawakilisha Wizara ya Afya Zanzibar Rashid Maulid Rashid amesema ujio wa kongamano hilo kwa Zanzibar ni chachu ya mafanikio katika kuwaeleza watafiti na wanasayansi kwamba zinapofanywa tafiti hazishii kuwekwa na zinafanyiwa kazi kwa maendeleo ya nchi.

Mapema waandaji wa Mktano huo walikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ambapo alisema kuwa Wizara ya Afya Zanzibar itashirikina na Tanzania Helth summit kuona kwamba kongamano hilo linakuwa na mafanikio makubwa Tanzania Bara visiwani.

Loading