Maadhimisho siku ya Maabara Duniani

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewataka wataalamu wa Maabara kuvifanyia utafiti vitu wanavyovichunguza ikiwemo maradhi ili kuyadhibiti kwa njia za kisayansi. Akisoma hotuba ya rais Mwinyi katika kilele cha wiki ya Maabara Duniani huko Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar, Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui, alisema, kufanya hivyo kutasaidia taasisi […]

WAUGUZI WATAKIWA KUWAJIBIKA KULETA MABADILIKO KATIKA SEKTA AFYA

WAUGUZI wanafunzi wametakiwa kuwajibika na kuhakikisha kuwa wanaleta  mabadiliko makubwa katika fani hiyo ili kuongeza hadhi na sifa za wauguzi hasa kwa walioko makazini. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika Mkutano Mkuu wa wa 18 na Kongamano la Kisayansi lilowashirikisha wanafunzi wauguzi katika vyuo vinane Tanzania Bara na Visiwani. […]

Wiki ya Maabara

WATAALAMU wa Maabara nchini wametakiwa kufanya kazi kwa pamoja katika kufanya uchunguzi wa maradhi na bidhaa nyengine kwa lengo la kuimarisha afya za wananchi. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh wakati alipofanya ziara maalaumu ya kutembelea maonesho ya wataalamu wa maabara mbali mbali yaliyofanyika katika viwanja nya Mapinduzi Square […]

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kujenga Nyumba za Makaazi kwa ajili ya Madaktari wa Hospitali za Wilaya

Serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itahakikisha inawawekea makaazi ya karibu watoa huduma wa afya katika Hospitali zote za Wilaya Unguja na Pemba ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi sambamba na kufika kazini kwa wakati Akizungumza na Mkandarasi pamoja na wasimamizi wa kampuni ya Rans inayojenga nyumba za Madaktar kaitkaH ya […]

HOSPITALI ya wilaya Kivunge kwa mara ya Kwanza imefanya upasuaji wa kutumia utaalamu wa matundu madogo (laparoscopy)

HOSPITALI ya wilaya Kivunge, mkoa wa Kaskazini Unguja, imefanya upasuaji wa kutumia utaalamu wa matundu madogo (laparoscopy) ambao ni wa kwanza kufanyika hospitalini hapo. Mkuu timu ya Madaktari ya Kichina, Profesa Jiang Guoqing, aliongoza kumfanyia upasuaji mgonjwa wa maradhi ya ngiri akisaidia na madaktari wazalendo katika hospitali hiyo. Akizungumza baada ya upasuaji huo, Profesa Guoqing, […]

Wataalamu wa Maabara wametakiwa kufanya uchunguzi wa maradhi kwa kufuata utaalamu uliopo duniani

WATAALAMU wa Maabara wametakiwa kufanya uchunguzi wa maradhi kwa kufuata utaalamu uliopo duniani kote ili kuweza kutolewa   tiba sahihi kwa wagonjwa. Akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo wataalamu wa maabara Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Salim Slim amesema wataalamu hao wanajukumu kubwa la kuchunguza maradhi kwa kina na kuweza kupatikana kwa tiba ya […]

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kupambana na maradhi ya Malaria na kuhakikisha kuwa yanaondoka hapa nchini

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kufanya jitihada kubwa ya kupambana na maradhi ya Malaria na kuhakikisha kuwa yanaondoka hapa nchini. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyaeleza hayo wakati alipofanya mazungumzo na Balozi Maalumu kutoka Taasisi African Leaders Malaria Alliance (ALMA) alipofika ofisini kwake Vuga Amesema Wizara ya Afya kwa kushirikina na Washirika […]

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itaanza kuhamisha huduma za uzazi katika Hospitali ya Mnazi mmoja ili kuweza kupisha ujenzi

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itaanza kuhamisha huduma za uzazi katika Hospitali ya Mnazi mmoja ili kuweza kupisha ujenzi, ukarabati na utanuzi wa Hospitali hiyo unaotarajiwa kuanza mwezi wa sita mwaka huu. Akitoa Taarifa kwa wananchi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema kutokana na kuanza kwa taratibu za utanuzi na ujenzi wa […]

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na Mashirika ya kimataifa kutokomeza Malaria Zanziabr

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na Mashirika ya kimataifa na wadau wengine kuhakikisha kuwa maradhi ya Malaria yanaondoka hapa nchini. Akifungua Mkutano wa siku moja wa Mpango Kazi kwa mwaka 2025 uliowashirikisha Wadau na Mashirika ya Kimataifa   Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Wizara  ya Afya Zanzibar  Dkt Salim Slim amesema jitihada zinafanyika […]

Loading