- UTANGULIZI.
Bohari ya Dawa ni moja kati ya taasisi za Wizara ya Afya yenye jukumu la kusaidia kukuza mfumo wa utoaji wa huduma za afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba zenye ubora unaotakiwa ili kufikia mahitaji ya wananchi wa Zanzibar kupitia vituo vya afya, hospitali za wilaya, mikoa na rufaa. Kabla ya mwaka 2011, Bohari ya dawa ilikuwa kitengo chini ya Mfamasia Mkuu. Katika kuiongezea Bohari uwezo wa kiutendaji, mwaka 2011 ilipewa hadhi ya kuwa Idara ikiwa na maghala mawili Maruhubi unguja na micheweni kisiwani Pemba.
Kwa sasa Bohari Kuu ya Dawa ina jukumu la kupokea, kuhifadhi na kusambaza dawa muhimu, vifaa tiba, vifaa vya uchunguzi wa kimaabara na uchunguzi wa mionzi, pamoja na kutoa taarifa mbali mbali za matumizi ya dawa kwa ajili ya kuisaidia Serikali kutoa maamuzi ya kufaa.
Bohari Kuu ya Dawa ni idara inayoongozwa na Mkurugenzi akisaidiwa na wakuu wa divisheni.
Bohari kuu ya dawa ina Divishen kuu 4 ambazo ni:-
- Divisheni ya huduma kwa wateja.
- Divisheni ya uthibiti wa viwango (Quality Assurance)
- Divisheni ya manunuzi na usimamizi wa mwenendo wa dawa
- Divisheni ya utawala na fedha.
KAZI ZA BOHARI
- Bohari kuu ya dawa ina jukumu la Kupokea dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa na serikali pamoja washirika mbalimbali wa maendeleo.
- Kusimamia uhifadhi na utunzaji dawa na vifaa tiba.
- Kusambaza dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya na hospitali zote za Unguja na Pemba kwa sasa inazambaza Dawa na Vifaa tiba kwa vituo 190 vya serikali na vya vikosi vya Ulizi na Usalama.
- Kusimamia mwenendo wa dawa na vifaa tiba katika vituo vyote vya afya na hospitali Unguja na Pemba.
- Kutoa mafunzo na miongozo mbalimbali juu ya uhifadhi na utunzaji wa dawa na vifaa tiba kwa wafamasia wa wilaya na watunza dawa katika vituo vya Afya na hospitali.