Blog

WHO WAKUTANA NA WATENDAJI WA AFYA ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema Wizara ya afya ina jukumu la kutoa huduma bora za afya Nchini kwa kulinda na kutibu ili kupunguza madhara mbalimbali yatokanayo na maradhi katika jamii. Ameyasema hayo huko Verde Mtoni katika mkutano wa pamoja kati ya WHO na Wizara ya Afya wa mapitio ya kukagua utekelezaji […]

MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLA AMEZINDUA WARSHA YA MAFUNZO YA UTOAJI HUDUMA KWA WAGONJWA WA SARATANI

Wananchi wametakiwa kubadilisha utaratibu wa Maisha kwa kutenga muda wa kufanya mazoezi na kula vyakula vyenye Afya ili kupunguza maradhi yasiyoambukiza Nchini ikiwemo Saratani. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa Kauli hiyo katika uzinduzi wa Warsha ya Mafunzo ya utoaji Huduma kwa Wagonjwa wa Saratani iliyofanyika Ukumbi wa Golden […]

SMZ NA SERIKALI YA OMAN YAKAGUA ENEO LINALOTARAJIWA KUJENGWA HOSPITAL YA MKOA MAHONDA

Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman inatarajia kujenga Hospitali ya Mkoa Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja ili kuondosha msongamano wa wagonjwa katika haspitali kuu ya Mnazimmoja. Akizungumza mara ya baada ya kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa Hospitali hiyo, Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui amesema lengo la […]

Mkutano wa watendaji wa afya mama na mtoto wafanyika Zanzibar

Wizara ya Afya imeamua kuchukuwa hatua madhubuti  na kuhakikisha wanaondosha changamoto zinazowakabili ili kupunguza vifo vya mama na mtoto nchini. Hayo amesema Mkurugenzi wa Kinga na elimu ya afya Dr. Ali Said Nyanga wakati akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili afya ya mama na mtoto huko ukumbi wa chuo cha utalii Marughubi Mjini Zanzibar. Amesema […]

Waziri Mazrui amefanya mazungumzo na hospital ya Benjamin Mkapa

Waziri wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara ya Afya ipo tayari kushirikiana na Hospital ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma katika kutoa huduma mbali mbali za matibabu. Amesema kutokana na huduma za matibabu wanazozitoa hospital hiyo ni zenye ubora zaidi Wizara ya Afya itafanya mashirikiano ili kuweza kupeleka wagonjwa walioshindikana kupata matibabu. Waziri Mazrui […]

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla azindua kampeni ya chanjo ya polio Mkokotoni

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka mkakati muafaka wa kupunguza watu wasio na kinga ili kufikia malengo ya kutokomeza ugonjwa wa Polio Nchini. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya kutoa Chanjo ya matone ya Pilio iliyofanyika katika Viwanja vya Mkokotoni Sokoni […]

WIZARA YA AFYA YAPOKEA MAGODORO NA MASHUKA KUTOKA DIASPORA

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmesd Mazrui akipokea msaada wa Magodoro na Mashuka kwaajili ya hospitali za Zanzibar, wenye thamani ya zaid ya shilingi milioni 13 kutoka kwa Wazanzibar waishio Nchi za Umoja wa falme za kiarabu (Diaspora) huko Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Unguja. Wizara ya Afya imepokea msaada wa mashuka na magodoro wenye […]

SHIRIKA LA AFYA DUNIANI(WHO)WATAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUFANIKISHA HUDUMA ZA AFYA ZANZIBAR

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na wawakilishi  kutoka  Shirika la Afya Duniani (WHO)  wakati walipofika ofisini kwake Mnazimmoja Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema litaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar katika kufanikisha huduma za afya nchini . Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi mkaazi  wa Shirika la Afya Duniani […]